Gowee

From Wikipedia, the free encyclopedia

Gowee
Remove ads
Remove ads

Gowee au kore ni ndege wa jenasi Corythaixoides katika familia Musophagidae. Jina lako linatoka sauti yao inayosikika kama “gwee” au “gowee” (Waingereza wasikia "go-away" na huitwa ndege hawa Go-away-bird). Huitwa shorobo pia kama spishi nyingine za Musophagidae.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Ndege hawa wana rangi ya kijivu na nyeupe na wana kishungi kirefu. Wanatokea Afrika chini ya Sahara. Hawawezi kupuruka vizuri sana lakini hukimbia juu ya matawi ya miti. Hula matunda hasa na majani na maua pia, na mara chache hukamata wadudu na koa. Hujenga tago lao kwa vijiti katika mti mwenye miiba, kama spishi ya Vachellia (mgunga) au Balanites (mjunju), na jike hutaga mayai 1-4 lakini 3 kwa kawaida. Vinda wakitoka kwa mayai, wanapambwa na malaika mazito na macho yao ni wazi tayari au karibu.

Remove ads

Spishi

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads