Shorobo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Shorobo
Remove ads
Remove ads

Shorobo, dura au huruvi ni ndege wa familia Musophagidae. Spishi za jenasi Corythaixoides zinaitwa gowee pia na Tauraco fischeri anaitwa kulukulu. Spishi za jenasi Corythaixoides na Crinifer zina rangi ya kijivu na nyeupe, nyingine zina rangi ya majani, nyekundu, buluu na zambarau. Shorobo ni ndege wa pekee ambao wana pigmenti ya rangi ya majani inayoitwa turacoverdin. Ndege hawa wanatokea Afrika chini ya Sahara. Hawawezi kupuruka vizuri sana lakini hukimbia juu ya matawi ya miti. Hula matunda hasa na majani na maua pia, na mara chache hukamata wadudu na makoa. Hujenga tago lao kwa vijiti na jike hutaga mayai 2 au 3. Vinda wakitoka kwa mayai, wanapambwa na malaika mazito na macho yao ni wazi tayari au karibu.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads