Kidudu-kifuko
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Vidudu-kifuko ni vidudu wadogo sana wa faila Cycliophora wanaoishi kwenye sehemu za mdomo za kambamawe. Hadi sasa wamefunua kwenye spishi tatu za kambamawe: kambamawe wa Marekani (Homarus americanus), kambamawe wa Ulaya (Homarus gammarus) na kambamawe wa Unowe (Nephrops norvegicus)[1].

Wapevu hutokea katika hatua mbili. Ile kubwa zaidi ni hatua ya kujilisha, ambayo ina urefu wa µm 350 na upana wa µm 120. Ina mwili unaofanana na kifuko na mdomo wenye mpare unaobeba minyiri na mkundu juu yake (tazama mchoro). Inashikamana na unywele wa kambamawe kwa njia ya sahani ya kunyonya. Katika hatua hii wanyama wanaweza kuzaa bila utungisho kwa kuchipua nakala za wenyewe[2].
Katika hatua ya ngono kuna jinsia mbili ambazo zote zina urefu wa µm 85 na upana wa µm 40. Dume hana mdomo, mkundu wala mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, lakini ana korodani mbili. Jike ana mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na yai moja. Baada ya utungisho, yai hukua na kuwa lava ambaye hufyonza mwili wa mama yake hadi ganda tu libaki. Kisha lava huogelea kwenda kutafuta mwenyeji mpya[2].
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads