Damiani Nam Myonghyok
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Damiani Nam Myonghyok (alifariki Seoul, 24 Mei 1839) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000 [1].
Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake kilichompata kwa kukatwa kichwa pamoja na Augustino Yi Kwanghon, Agatha Kim A-gi, Magdalena Kim Obi, Barbara Han A-gi, Ana Pak A-gi, Agatha Yi So-sa, Lusia Pak Hui-sun na Petro Kwon Tugin[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads