Mdudu Mikia-miwili
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wadudu mikia-miwili ni wadudu wadogo bila mabawa wa nusungeli Diplura (ngeli kufuatana na wataalamu wengi) katika nusufaila Hexapoda walio na mikia miwili ambayo siyo mikia kweli lakini serki (cerci) ndefu. Wana kiwiliwili kilichorefuka chenye urefu wa mm 2-5 (spishi kadhaa za jenasi Japyx zinaweza kufika mm 50). Hawana macho lakini wana vipapasio vyenye pingili 10 au zaidi kama shanga. Kiwiliwili hakina pigmenti isipokuwa serki nyeusi katika spishi kadhaa. Fumbatio inabeba vilengelenge vinavyofyonza unyevu kutoko mazingira (kama collophore kwa wadudu mkia-fyatuo). Wadudu hawa wanatokea katika udongo mnyevu, majani yaliyoanguka ardhini na mboji, na hula arithropodi wadogo sana, kuvu na maada ya viumbehai.
Remove ads
Picha
- Spishi ya Campodeidae
- Japyx solifugus
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads