Dogo Janja

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Abdulaaziz Chande (anajulikana kwa jina la kisanii Dogo Janja, alizaliwa tarehe 15 Septemba mwaka 1994) ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka Tanzania.

Ukweli wa haraka Abdulaaziz Chande, Pia anajulikana kama ...

Alizaliwa na kukulia katika kata ya Ngarenaro katika jiji la Arusha. Kwa sasa anaishi katika jiji la Dar es Salaam.

Remove ads

Wasifu

Alianza kuvutiwa na muziki mapema, lakini aliachia kazi yake ya kwanza mwaka 2016 aliposaini mkataba na Kundi la Tip Top Connection, lililoanzishwa na Babu Tale, ambalo hapo awali lilikuwa na wasanii maarufu wa Bongo Flava kama Rayvanny. Albamu yake ya kwanza, My Life, ilitoka mwaka 2016 na ilipokelewa vyema, na hivyo kumfanya kujulikana kama msanii.[1]

Tuzo na mafanikio

  • Tuzo za Muziki Tanzania (KTMA) - Ameshiriki mara kadhaa lakini hakushinda rasmi hadi sasa.
  • African Entertainment Awards (AEAUSA) - Ameteuliwa kwenye baadhi ya vipengele, lakini rekodi kamili ya ushindi haijawekwa wazi.
  • Heshima ya Ushiriki Wake Katika Muziki wa Hip Hop Tanzania - Anatambulika sana kama mmoja wa wasanii bora wa kizazi kipya.

Maisha binafsi

Dogo Janja alimuoa msanii na mwigizaji maarufu Irene Uwoya mwaka 2017, jambo ambalo lilizua gumzo kubwa mitandaoni kutokana na tofauti yao ya umri. Hata hivyo, ndoa yao haikudumu muda mrefu, na walitengana kimya kimya baadaye. Kwa sasa maisha yake ya mahusiano yamekuwa ya siri zaidi, na hajakuwa akizungumzia waziwazi kuhusu uhusiano mpya. Irene Uwoya,[2] mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz.[3]

Diskografia

Albamu

  1. Tatizo Pesa

Nyimbo:[4]

  • 2016: My life
  • 2017: Ngarenaro
  • 2017: Ukivaaje Unapendeza
  • 2018: Banana
  • 2018: Mikogo Sio
  • 2018: Wayu Wayu
  • 2018: Since Day One
  • 2019: Yente
  • 2020: Asante ft Lady Jaydee
  • Asante Mama

Albamu iliyotolewa mwaka 2021, ikiwa na nyimbo kama 'My Life' na 'Umenishinda'.

  • Sitaki

Wimbo uliotolewa mwaka 2021.

  • Kilimanjaro

Wimbo uliotolewa mwaka 2023 akimshirikisha msanii Loui.

  • Vunja Mifupa

Wimbo uliotolewa mwaka 2024

  • Kindumbwe

Wimbo mwingine wa mwaka 2024

  • Kindumbwe

Wimbo mwingine wa mwaka 2024

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads