Irene Uwoya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Irene Pancras Uwoya (alizaliwa 18 Desemba 1988) ni mwigizaji na mwongozaji wa filamu, mwanamitindo wa zamani na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania. Irene pia alishiriki mashindano ya "Miss Tanzania" na kushika nafasi ya tano mwaka 2006/2007 [1][2]
Remove ads
Alifahamika sana kwa uhusika wa "Oprah" (2008) alioshiriki na Steven Kanumba na Vincent Kigosi. Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Uliyemchokoza Kaja, Figo, Rosemary, Snitch, The Return of Omega na Money.
Uwoya alianza shule ya msingi Mlimwa kisha akahamia Shule ya Bunge iliyopo Dar-es-Salaam kwa ajili ya elimu ya upili. Baadaye akaenda Greenville jijini Kampala, Uganda.[3][4]
Kwenye mwezi Oktoba 2017, habari zilitapakaa katika mitandao mbalimbali nchini Tanzania kuwa Uwoya ameolewa na Dogo Janja - msanii wa hip-hop Tanzania.[5] Siku kadhaa mbele kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya alithibitisha kuolewa na Dogo Janja.[6]
Remove ads
Baadhi ya filamu zake
- Uliyemchokoza Kaja
- Figo
- Rosemary
- Snitch
- The Return of Omega
- Money Talk
- Nyati
- Omega Confusion
- Question Mark
- Apple
- Safari
- Zawadi Yangu
- Innocent Case
- Nyota Yangu
- Last Card
- Doa la Ndoa
- Ngumi ya Maria
- Baamed
- Sobbing Sound
- Mtihani
- Chupa Nyeusi
- Dj Ben
- Senior Bachelor
- Kiapo
- Eagle Eyes
- Diversion of Love
- Off Side
- Fair Decision
- Pretty Girl
- My Dreams
- Peace of Mind
- Damu Moja
- Shakira
- Oprah
- Yolanda
- Tanzanite
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads