Dorotheo wa Turo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dorotheo wa Turo (Antiokia ya Siria, leo nchini Uturuki, 255 hivi - Varna, Bulgaria, 362) alikuwa askofu wa mji huo wa Lebanoni [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Maisha
Dhuluma ya kaisari Diocletian ilimlazimisha kukimbia alipokuwa padri maarufu kwa elimu yake, lakini baadaye akarudi.
Alishiriki mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325, lakini alifukuzwa na kaisari Juliani Mwasi akakae Odyssopolis (Varna, leo nchini Bulgaria) kwenye Bahari Nyeusi. Huko alifia dini yake akiwa na umri wa miaka 107[4].
Maandishi
Anasemekana kuwa mwandishi wa kitabu "Matendo ya Wanafunzi Sabini" waliotumwa na Yesu kadiri ya Injili ya Luka 10:1.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads