Dutwa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dutwa ni kata na tarafa ya Wilaya ya Bariadi katika Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39117 [1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 29,519 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,792 waishio humo.
Historia
Eneo la tarafa ya Dutwa lilikuwa utemi katika tawala za jadi za jamii ya Wasukuma. Utemi huo ulianzishwa na ukoo wa Wahunda waliotokea kitongoji cha Bugunda, leo Wilaya ya Sikonge katika mkoa wa Tabora.
Mtemi wa kwanza aliitwa Gamaleka; mpaka sasa jumla ya watemi 27 wameshatawala Dutwa. Mtemi wa mwisho ni John Kasili. Orodha ya watemi ni kama ifuatavyo: Gamaleka, Sangulilu, Gambimeda, Mabera, Itobya, Nyasilu, Sagayika, Gilya, Balina, Lusha, Liswa, Galidi, Mushuda, Ileme, Buyunge, Mlola, Kasili, John.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads