Mkoa wa Simiyu

kanda ya Ziwa, Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Simiyu
Remove ads

Mkoa wa Simiyu ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Ulianzishwa rasmi Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Shinyanga upande wa mashariki[1]. Eneo lake ni la km2 25,212. Unapakana na mikoa ya Mara upande wa kaskazini, Arusha upande wa mashariki, Shinyanga na Singida upande wa kusini, Mwanza upande wa magharibi. Ndani ya eneo lake kuna sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo imeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia. Kadiri ya sensa ya mwaka 2022, mkoa una wakazi 2,140,497 [2]. Makao makuu yako Bariadi.

Thumb
Mahali pa mkoa nchini Tanzania.

Mkoa una postikodi namba 39000 [3]

Remove ads

Wakazi

Kadiri ya sensa ya mwaka 2022, mkoa una wakazi 2,140,497 [4] kutoka 1,584,157 wa mwaka 2012, [5] walipokuwa wameongezeka 1.8% kwa mwaka katika miaka 2002-2012[5].

Msongamano wa watu ulikuwa 63 kwa kilomita mraba.[5]

Kabila kubwa ni lile la Wasukuma.

Wilaya

Mkoa huo mpya una wilaya 6 zifuatazo: Bariadi Mjini, Bariadi, Busega, Maswa, Meatu, Itilima.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads