Elizabeth Michael

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Elizabeth Michael (maarufu kama Lulu; amezaliwa 16 Aprili 1995) ni mwigizaji wa filamu kutoka Tanzania. Mwaka wa 2013 alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival kama msanii bora wa kike kupitia filamu "Foolish Age". Mwaka 2017 alitajwa na Tuzo za Vijana Afrika zifanyikazo nchini Ghana miongoni mwa vijana 100 wa Afrika wenye ushawishi mkubwa.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Majina mengine ...
Remove ads

Maisha ya awali

Elizabeth alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam Tanzania. Ni mtoto wa Lucrecia Kalugira na Michael Kimemeta.

Baadaye alijiunga katika shule ya Remnant Academy ambapo alimaliza elimu ya msingi. Alipata kusoma Perfect Vision High School, St Mary's High School kwa ajili ya Elimu ya sekondari. Baadaye alijiunga katika Chuo Cha Utumishi Wa Umma Tanzania (TPSC) akisomea kozi ya stashahada ya Rasilimali watu na Utawala (Diploma In Human Resources Management).

Remove ads

Kazi

Uigizaji

Alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka mitano mnamo mwaka 2000. Baadae alijiunga na kikundi cha Sanaa Kaole Group ambapo alikuwa pamoja na Steven Kanumba, Vincent Kigosi, Mwanaidi Suka na wengine wengi ambapo aliigiza tamthilia nyingi za runinga kama vile Gharika, Taswira, Zizimo na nyingine nyingi ambapo alikuwa akitumia jina la Lulu ambalo limekuwa maarufu mpaka leo.

Baadae alianza kuigiza filamu akiwa bado na Umri mdogo,a mbapo filamu yake ya kwanza ilikuwa Misukosuko akishirikiana na Jimmy Mponda. Mnamo mwaka 2006 aliigiza filamu iitwayo wema iliyoandaliwa na Game 1st Quality na badae filamu nyingine nyingi kama Family Tears,Ripple Of Tears,Passion,Dangerous Girl na nyingine nyingi.Mpaka sasa amepata kuigiza filamu zaidi ya thelathini.

Pia amepata kufanya Igizo la redioni lililoitwa Wahapahapa Akitumia jina la Mainda. lililoandaliwa na Media For Development International wakishirikiana na Ubalozi wa Marekani,Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na chuo cha Johns Hopkins University Center For Communication Programs cha Marekani Igizo hilo liliongozwa na mmarekani afanyaye shughuli zake Afrika Bwana Jordan Riber.

Pia Katika mradi huohuo wa Wahapahapa alipata kuigiza katika Video mbili za wasanii Lady Jay Dee iitwayo Shamba na Ya Enika iitwayo Changanya. Mradi wa Wahapahapa ulikuwa na lengo la kuelimisha jamii juu Ya malezi bora Ya mtoto katika kipindi cha ukuaji.

Mnamo August 2013 Lulu alizindua filamu Yake Iitwayo Foolish Age ambayo Ni filamu Yake ya kwanza kuitaarisha mwenyewe.Ilizinduliwa katika ukumbi wa Mlimani City uliopo Dar Es Salaam Na kuhudhuriwa Na mamia ya Watu.Foolish Age ilifanya vizuri sokoni Na ilipata kuonyeshwa katika Tamasha Kubwa La Kimataifa La Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), na baadae kuteuliwa kuwania Filamu Inayopendwa na Lulu alishinda Muigizaji wa Filamu Wa Kike Anaependwa kupitia filamu hio katika Tuzo za Watu 2014.

Mnamo Mwaka 2015 Alizindua Filamu Yake ya pili Kama mtayarishaji iitwayo Mapenzi Ya Mungu. Filamu Hio ilionyeshwa katika Tamasha La Filamu La Kimataifa La Zanzibar (ZIFF) na mwaka 2016 ilishinda Filamu Bora Afrika Mashariki katika Tuzo Za Africa Magic Viewers Choice Awards zilizofanyika Lagos Nigeria.

Utangazaji

Amewahi Kuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga kiitwacho watoto wetu Kinachorushwa na Runinga Ya ITV Tanzania Akiwa na umri mdogo mnamo mwaka 2004-2007.

Pia mnamo mwaka 2014 na 2015 alikuwa mtangazaji wa mashindano Ya kutafuta vipaji vya uigizaji Tanzania yaitwayo Tanzania Movie Talents.

Remove ads

Ubalozi na Matangazo

  • 2013/14 alichaguliwa Kuwa balozi wa tamasha la filamu liitwalo Dar Film Festival lililofanyika Dar es Salaam.
  • 2015 alifanya kazi na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kama mtangazaji wa kipindi cha Airtel Yatosha Tv Show.
  • Pia ni balozi wa kampuni ya Paisha Tanzania, ijushughulishayo na ufanyaji wa biashara mitandaoni
  • Pia aliteuliwa na kampuni ya Hengan Baby Products and Sanitary co ltd Kuwa balozi wa freestyle napkins bidhaa za wanawake kwa miaka miwili
  • Pia ni balozi wa Sinema Zetu International Film Festival tamasha la filamu linaloandaliwa Na chaneli ya Sinema Zetu ya kampuni ya Azam
  • Pia ni balozi wa Azania inajulikana kama pishi la Lulu, ni manager wa upcoming actor ajulikanae kama Suhelyht khan ambae jina lake halisi ni Suhely Tarmohammed.

Filamugrafia

Tamthilia

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Igizo la radio

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka, Filamu ...

Kama mtayarishaji

  • Foolish Age
  • Mapenzi Ya Mungu
  • Ni Noma
Remove ads

Tuzo Alizoshinda

  • 2013 Zanzibar International Film Festival- Mwigizaji Bora wa Kike
  • 2014 Tuzo za watu - Mwigizaji wa Kike Anayependwa
  • 2016 Africa Magic Viewers Choice Awards- Filamu Bora Afrika Mashariki (Mapenzi Ya Mungu)
  • 2016 Swahili Fashion Week Awards - Style Icon Of The Year

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads