Embakomu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Embakomu (Abba 'Ěnbāqom; 1470 hivi - 1565 hivi) alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia,[1] tena mwandishi na mtafsiri wa vitabu [2], k.mf., wa Anqaṣa Amin.[3]

Kama abati wa monasteri muhimu ya Debre Libanos aliitwa Echage, cheo cha pili katika Kanisa hilo, na mkuu wa monasteri zote za Ethiopia, akatazamwa kama mtu mwenye athari kubwa zaidi katika Kanisa kwa sababu askofu alikuwa Mmisri[4], si mwenyeji kama kawaida ya Echage.[5][6][7]

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Aprili.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads