Engaruka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Engaruka ni kata ya Wilaya ya Monduli katika Mkoa wa Arusha, Tanzania yenye postikodi namba 23415.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 17,087 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,121 [2] walioishi humo, wengi wakiwa Wamasai.
Iko kaskazini kwa Mto wa Mbu, karibu na barabara ya kwenda Oldonyo Lengai.
Historia
Katika eneo lake yanapatikana maghofu maarufu ya ustaarabu wa zama za chuma (karne ya 15 hadi katikati ya karne ya 18) ulioendeleza kilimo cha umwagiliaji[3][4] pamoja na kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kuiongezea samadi.
Utafiti unaelekea kusema walikuwa maelfu ya watu wa jamii ya Kikushi kama Wairaqw[5][6][7][8].
Wakulima hao walijenga kijiji kwenye miteremko ya eneo la Bonde la Ufa, ambacho kiilikuwa na maelfu ya watu.
Walibuni mifumo bora na imara ya kilimo cha umwagiliaji; mifumo hiyo ilikuwa ikipitisha maji kutoka kwenye miinuko hadi kwenye matuta ya mazao.[9][10]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads