Mkoa wa Arusha

Mkoa nchini Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Arusha
Remove ads

Mkoa wa Arusha ni mojawapo ya mikoa ya Tanzania uliopo kaskazini mwa nchi. Unapakana na Kenya upande wa kaskazini na mkoa wa Kilimanjaro na mkoa wa Manyara upande wa kusini na magharibi, pia mkoa wa Shinyanga na mkoa wa Mara. Makao makuu ya mkoa ni jiji la Arusha, ambalo ni kitovu cha utalii na biashara kwa kuwa kando yake kuna mbuga maarufu za wanyama kama Serengeti, Ngorongoro, na Mlima Kilimanjaro. Mkoa huo unajivunia utalii mkubwa unaochangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wake, pamoja na kilimo na viwanda vidogo. Mkoa wa Arusha una historia ndefu ya tamaduni mbalimbali zinazochangia utofauti wake wa kijamii na kiutamaduni.

Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...

Wakazi ni 2,356,255[2].

Remove ads

Eneo

Eneo lake ni km za mraba 34,526 zikiwemo km² 707 za maji ya ndani.[3].

Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani, kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara.

Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini, Ngorongoro na Karatu.

Makao makuu yapo Arusha mjini.

Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (m 2,878) ni volkeno hai bado, na mlima Meru ni volkeno iliyolala tangu mwaka 1910.

Mvua hunyesha kati ya milimita 1,800 kwa mwaka mlimani Arusha hadi mm 508 kwa mwaka katika maeneo makavu.

Remove ads

Uchumi

Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Tarangire ziko karibu.

Barabara ya lami Dar es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi.

Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti.

Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.

Kati ya wakazi asili wa mkoa ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamasai.

Remove ads

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads