Epafra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Epafra (kwa Kigiriki Ἐπαφράς, Epafras; alifariki Kolosai, 80) alikuwa mwanafunzi na msaidizi wa Mtume Paulo katika uinjilishaji wa mji wa Efeso na mkoa wa Asia.

Inaonekana alikuwa mwenyeji wa Kolosai na alitumwa kueneza Ukristo huko (Kol 1:7; 4;12-13) pamoja na Laodikea na Yerapoli.
Baada ya muda, yalijitokeza huko matatizo ya kiimani yaliyomfanya Paulo aandike barua maarufu kama Waraka kwa Wakolosai.
Paulo anamtaja pia kama mfungwa mwenzake (Waraka kwa Filemoni 1:23).
Kwa jinsi alivyomsifu, kama mshiriki mpenzi wa kazi yake na mtumishi mwaminifu wa Kristo, tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi kama mtakatifu[1].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads