Espagathus wa Lyon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Espagathus wa Lyon ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Lyon wanaoheshimiwa kama watakatifu[1].
Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lugdunum (siku hizi Lyon).
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Juni[2], pamoja na wenzake 47: askofu Potinus wa Lyon na mtumwa bikira Blandina wa Lyon, Aleksanda, Attalus, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia. Baadhi walifia gerezani, baadhi waliuawa katika kiwanja cha michezo mbele ya maelfu ya watazamaji, ama kwa kwa kukatwa kichwa ama kwa kutupwa waliwe na wanyamapori.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads