Potinus wa Lyon

From Wikipedia, the free encyclopedia

Potinus wa Lyon
Remove ads

Potinus (kwa Kifaransa Pothin; Frigia, katika Uturuki wa leo, 87 - Lyon, katika Ufaransa wa leo, 177) alikuwa askofu wa Lyon aliyeuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo.

Thumb
Kanisa la Mt. Potinus huko Lyon.

Askofu Ireneo alimtaja kama mtangulizi wake mjini Lyon katika barua ambayo anadhaniwa kuwa aliwaandikia Wakristo wa mkoa wake wa asili, Asia Ndogo, ili kueleza majaribu yaliyowapata.

Kadiri yake, Potinus alitumwa na Polikarpo wa Smirna kufanya umisionari Ulaya magharibi pamoja na Wakristo wengine.

Anahesabiwa kuwa askofu wa kwanza wa Ufaransa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini kwa kuwa akiwa na umri wa miaka 90 alifariki mara baada ya kufungwa gerezani.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Juni[2] pamoja na wenzake 47: mtumwa bikira Blandina wa Lyon, Aleksanda, Attalus, Vezi Espagati, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, Jeminiani, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia. Baadhi walifia gerezani kama yeye, baadhi waliuawa katika kiwanja cha michezo mbele ya maelfu ya watazamaji, ama kwa kwa kukatwa kichwa ama kwa kutupwa waliwe na wanyamapori.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads