Europi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Europi (Europium) ni elementi ya kikemia yenye alama Eu na namba atomia 63, maana yake kuna protoni 63 katika atomu. Europi imepangwa kwenye jedwali la elementi katika kundi la lanthanidi. Ni elementi inayotendana haraka sana na hewa au unyevu, hivyo inahitaji kutunzwa ndani ya viowevu visivyotendana nayo.
Europi ni metali laini sana: inaweza kukatwa kwa kisu. Kama haikuoksidika rangi yake ni nyeupe ya kung'aa.
Ilisafishwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1901 ikapewa jina la bara la Ulaya (Europa). [1]
Matumizi ya europi hutumia tabia ya mmemetuko (phosphorescence) wa kampaundi zake. Ni elementi adimu.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads