Eusebi wa Samosata

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Eusebi wa Samosata (alifariki Dolikha, leo Dülük, Uturuki, 379 hivi) alikuwa askofu wa Samosata kuanzia mwaka 361 hadi kifodini chake.

Thumb
Picha takatifu wa Mt. Eusebi.

Alidhulumiwa na Dola la Roma kwa kupinga Uario ulioungwa mkono na makaisari. Chini ya Konstanti II aliimarisha waumini wake katika imani sahihi kwa kuwatembelea huku amevaa kama askari, halafu chini ya Valens alipelekwa uhamishoni huko Thrakia [1][2].

Hatimaye, kisha kupatikana tena amani kwa Kanisa Katoliki chini ya Theodosi Mkuu, aliuawa na mwanamke wa madhehebu hayo aliyemrushia kigae kichwani[3][4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Juni[5].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads