Filogoni wa Antiokia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Filogoni wa Antiokia (alifariki Antiokia, leo nchini Uturuki, 324) alikuwa askofu mkuu wa mji huo kuanzia mwaka 314 hadi kifo chake.
Kwanza alioa na kuzaa binti; alikuwa wakili maarufu kwa kutenda haki.
Baadaye aliitwa na Mungu kushika uongozi wa jimbo na kupinga Uario akitetea imani sahihi pamoja na Aleksanda I wa Aleksandria na wengineo.
Hatimaye alifungwa kwa ajili ya imani katika dhuluma ya kaisari Licinius.
Yohane Krisostomo alimsifu kwa stahili zake katika hotuba maarufu[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 20 Desemba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads