Fransisko Borja

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fransisko Borja
Remove ads

Fransisko Borja, S.J. (Valencia, Hispania, 28 Oktoba 1510 - Roma, Italia, 30 Septemba 1572) alikuwa padri wa Shirika la Yesu aliyeliongoza kama mkuu wa tatu kuanzia mwaka 1565 akiwa na mafanikio makubwa.

Thumb
Mt. Fransisko Borja.

Kitukuu wa Papa Aleksanda VI, aliwahi kuoa na kuzaa watoto wanane, ila alipofiwa mke wake aliacha vyeo vyake vya kidunia na kukataa vile vya kidini, akaingia utawani (1546) alipong'aa kwa maisha magumu na roho ya sala[1].

Koo nyingi za kifalme Ulaya zinachanga damu yake.

Papa Urbano VIII alimtangaza mwenye heri tarehe 23 Novemba 1624, halafu Papa Klementi X akamtangaza mtakatifu tarehe 20 Juni 1670.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Muziki

  • Marc-Antoine Charpentier, Motet pour St François de Borgia, H.354, for 1 voice, 2 treble instruments, and continuo (? late 1680s)

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads