Fransisko Solano

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fransisko Solano
Remove ads

Fransisko Solano, O.F.M. (jina la Kihispania kwa kirefu lilikuwa: Francisco Sánchez-Solano Jiménez; Montilla, Córdoba, Andalusia, Hispania, 10 Machi 1549 - Lima, Peru, 14 Julai 1610) alikuwa mtawa wa urekebisho wa Wareformati wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki. kutoka Hispania na mmisionari huko Amerika Kusini.

Thumb
Mt. Fransisko Solano na mwananchi wa Tucuman walivyochorwa na mtu asiyejulikana mwaka 1588 hivi. Miguuni pake ala ya muziki aliyoitumia kwa kawaida katika uinjilishaji.
Thumb
Mt. Fransisko Solano na fahali kadiri ya Murillo.

Alifanya kazi ya kuhubiri na kueneza imani ya Kikristo katika maeneo mbalimbali ya Amerika Kusini, akijulikana kwa ufanisi wake wa kiroho na huruma kwa wahitaji.[1]

Ili kuokoa watu alifanya umisionari katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini, akihubiri na kutoa ushuhuda wake kwa Waindio na kwa wakoloni pia upya wa maisha ya Kikristo[2].

Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Juni 1675, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Desemba 1726.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Julai[3].

Remove ads

Sala yake

Yesu mwema, mkombozi na rafiki yangu!

Nina kitu gani usichonipa wewe? Najua nini usiyonifundisha wewe?

Nina thamani gani usipokuwa nami?...

Ndiwe uliyeniumba, tena bila ya kuniuliza. Wewe umeniumba.

Elekeza macho yako kwangu, Bwana, na unihurumie, kwa kuwa mimi ni mkiwa na maskini...

Kwa nini, Bwana Yesu wangu, wewe umesulubiwa, nami nasaidiwa na watumishi wako?

Kwa nini wewe uchi, nami nina vazi?

Kwa nini wewe umepigwa makofi na kutiwa taji la miba, nami nimepewa vitu vyema na kufarijiwa na fadhili nyingi?...

Mungu wa roho yangu, utukuzwe kwa yale uliyonijalia!

Bwana wangu, nafurahi kwamba u Mungu; jinsi hilo lilivyo zuri!

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads