Fransisko wa Laval
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fransisko wa Laval (Montigny-sur-Avre, Perche, 30 Aprili 1623 - Quebec, 6 Mei 1708), alikuwa askofu Mfaransa, wa kwanza katika koloni la New France, ambayo sasa ni sehemu ya Québec, Kanada, na mwanzilishi wa Shirika La Notre Dame wa Montreal.

Aliweka makao makuu katika jiji la Quebec na kwa miaka 50 hivi alistawisha Kanisa Katoliki katika Amerika Kaskazini hadi ghuba ya Meksiko[1].
Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Yohane Paulo II tarehe 22 Juni 1980, halafu mtakatifu na Papa Fransisko 3 Aprili 2014.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
