Gadolini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Gadolini
Remove ads
Remove ads

Gadolini (Gadolinium) ni elementi ya kikemia yenye alama Gd na namba atomia 64. Gadolini ni metali yenye rangi nyeupe-ya kifedha wakati haijaoksidika bado. Gadolini humenyuka na oksijeni ya hewani au unyevu polepole ikiunda mpako mweusi. Chini ya °C 20 ina tabia za kisumaku.

Kiasili hupatikana hasa kwa umbo la oksidi.

Jina lake limetokana na madini ya gadoliniti inamopatikana; madini yalipewa jina kwa heshima ya moja ya madini ambayo gadolinium hupatikana, yenye jina kwa mwanakemia Johan Gadolin kutoka Uswidi.

Gadolinium ina tabia kadhaa zisizo kawaida. Katika kampaundi za feleji nyongeza ndogo ya Gadolini hupunguza hupunguza utendanaji wake na oksijeni katika hali ya joto.[ <span title="This claim needs references to reliable sources. (June 2019)">onesha inahitajika</span> ]

Kampaundi za gadolini hutumiwa katika mikrowevu, uzalishaji wa diski za kompyuta na pia kwa skrini za rada.

Thumb
Sampuli ya madini ya gadolini.

Upatikanaji katika ganda la Dunia ni takribani miligramu 6.2 kwa kila kilogramu. Huchimbwa hasa China, Marekani, Brazil, Sri Lanka, Uhindi na Australia. Uzalishaji wa gadolini safi duniani ni karibu tani 400 kwa mwaka. [1] [2]

Remove ads

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads