Gairo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gairo ni makao makuu ya Wilaya ya Gairo katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67700.
Gairo uko kwenye barabara kuu ya Dodoma hadi Dar es Salaam na ni kituo cha kupitisha mizigo, pamoja na kituo cha kusafirisha mazao ya kilimo cha wilaya hiyo.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 12,684 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kata ya Gairo ilikuwa na wakazi wapatao 33,209, wengi wao wakiwa Wakaguru. [2] Kufikia 2002, idadi ya wakazi wa mji ilikuwa 16,982,[3]
Remove ads
Maendeleo
Gairo ni mmojawapo kati ya miji ambayo inakua sana nchini na unajulikana kwa kuwa unazalisha mazao ya biashara na chakula kama vile viazi vitamu, mahindi, maharagwe na vilevile kwa ufugaji.
Kutokana na ukaribu wake na barabara kuu ya Dodoma, mji wa Gairo umekuwa kati ya walishaji wakubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Hapo zamani Gairo ilikuwa chini ya jimbo la uchaguzi la Kilosa, baadaye ulipata kuwa jimbo linalojitegemea.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads