Gentile wa Fabriano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gentile wa Fabriano (1370 hivi – 1427) alikuwa mchoraji wa Italia aliyefanya kazi hasa katika mkoa wa Toscana.


Michoro yake maarufu zaidi inawahusu Yesu na Bikira Maria, nayo ni Ibada ya Mamajusi (1423) na Kukimbilia Misri.
Maisha
Gentile alizaliwa Fabriano, katika dola la Papa, (leo mkoa wa Marche).
Kabla ya mwaka 1380 mama yake alifariki, na hapo baba yake, Niccolò di Giovanni Massi, alijiunga na monasteri, alipofariki mwaka 1385. Hakuna habari zaidi kuhusu malezi yake.
Mwaka 1405 hivi, Gentile alikuwa akifanya kazi huko Venice, halafu akachora huko Fabriano, Foligno, Brescia, halafu tena Fabriano.

Tarehe 6 Agosti 1420 alikuwa Florence, halafu Siena, Orvieto na hatimaye mwaka 1427 alifika Roma, alipopata agizo la Papa Martin V, lakini hakumaliza kulitekeleza kwa sababu alifariki kabla ya tarehe 14 Oktoba.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads