George Floyd
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
George Floyd (1973 - 25 Mei 2020) alikuwa Mmarekani Mweusi kutoka Minnesota aliyefariki dunia kufuatia askari polisi mweupe wa Minneapolis, aliyejulikana kwa jina la Derek Chauvin[1] kumbana Floyd kwa kupiga goti juu ya upande wa nyuma wa shingo ya Floyd kwa muda wa takribani dakika 8 na sekunde 46 kadiri ya maelezo yaliyomo kwenye faili la malalamiko ya jinai lilofunguliwa dhidi ya Chauvin.[2][3].

Remove ads
Kifo chake
Mnamo 25 Mei, 2020, George Floyd aliuawa katika jiji la Minneapolis nchini Marekani na Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu mwenye umri wa miaka 44.[4] Floyd alikamatwa kwa tuhuma za kutumia noti ghushi ya $20. Chauvin alipiga magoti kwenye shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika tisa huku Floyd akiwa amefungwa pingu na kulala kifudifudi barabarani.[5][6][7] Maafisa wengine wawili wa polisi, J. Alexander Kueng na Thomas Lane, walimsaidia Chauvin kumzuia Floyd.[8] Lane pia alikuwa ameelekeza bunduki kwenye kichwa cha Floyd kabla ya Floyd kufungwa pingu. Afisa wa nne wa polisi, Tou Thao, aliwazuia watu waliokuwa karibu na eneo hilo kuingilia kati.[9]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
