Gesi miminika

From Wikipedia, the free encyclopedia

Gesi miminika
Remove ads

Gesi miminika (kwa Kiingereza: liquefied natural gas; kifupi: LNG) ni gesi asilia katika hali ya kiowevu au miminika. Ni dutu safi isiyo na rangi na isiyo na sumu,[1] inayotengenezwa kwa kupoza gesi asilia hadi nyuzi joto -160ºC hadi kiwango ambacho inakuwa kimiminika. Mchakato huo hurahisisha usafirishaji wenye ufanisi wa gesi asilia kwa kutumia barabara (malori) au bahari (meli).[2] Sababu kuu ya kupoza gesi ni, gesi miminika ina ujazo mdogo mara 600 kuliko gesi asilia ikiwa katika hali ya kawaida.[3]

Thumb
Meli za kubeba gesi miminika mara nyingu hutambuliwa kutokana na matangi ya mviringo
Thumb
Njia ya gesi miminika kutoka chanzo hadi mteja
Remove ads

Uzalishaji

Asilimia kubwa ya gesi asilia hukatama kwenye chanzo na kusafirishwa kwa njia ya bomba baada ya kuisafisha hadi kufikia hali ya methani safi kiasi[4]. Pasipo mabomba ni muhimu kupunguza ujazo wa gesi hii ili kuisafirisha ama kwa meli au kwa malori.[5]

Hadi mwaka 2012, duniani kote kulikuwa na vituo 20 vya kuzalisha na kusafirisha nje gesi miminika, vituo 63 vya kuingiza gesi miminika ndani ya nchi, na takriban meli 300 za kubeba gesi ya kimiminika zote zikiwa na uwezo wa kubeba tani za meta milioni 750 za gesi ya kimiminika kila mwaka. Kiasi hicho kinatarajiwa kuongezeka sana kwa kipindi cha miaka kumi ijayo kutokana na umaarufu unaoongezeka wa chanzo hicho safi cha kuwashia moto.[6]

Remove ads

Uchumi

Ujengaji wa mitambo ya gesi miminika unahitaji mtaji mkubwa na yenye madeni makubwa.[7] Lakini wakati gesi miminika ina gharama kiasi kuizalisha, maendeleo ya teknolojia yanapunguza gharama hizo zinazotokana na kuifanya kimiminika na kuirudisha tena katika hali yake ya gesi asilia.[8] Chapisho la BP World Energy Outlook lilitabiri mnamo mwaka 2012 kwamba biashara ya gesi miminika itakua kwa haraka maradufu kama ulivyokua haraka uzalishaji wa gesi asilia duniani, yaani kwa kiwango cha asilimia 4.4 kwa mwaka.[9]

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads