Gesi asilia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Gesi asilia
Remove ads

Gesi asilia ni gesi inayopatikana katika ardhi na inayotumiwa na binadamu kama fueli.

Thumb
Uzalishaji wa gesi asilia duniani

Tabia za gesi asilia

Kikemia ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali kama methani zilizotokana na kuoza kwa mata ogania kama mimea ya miaka mingi iliyopita.

Gesi asilia inapatikana katika ardhi yenye mwamba wenye vinyweleo vingi ulioko chini ya ganda la mwamba imara zaidi unaozuia gesi kupanda juu zaidi.

Ni fueli kisukuu ambayo ni muhimu kwa matumizi ya kibinadamu katika injini za kutengeneza umeme na pia kwa kuongeza joto katika nyumba za watu kwenye nchi zenye baridi.

Kwa matumizi ya kibinadamu gesi asilia hukamatwa kwenye chanzo chake. Baadaye inasafishwa kwa kuondoa maji na hidrokaboni mbalimbali ili kufikia kiwango cha juu cha methani cha asilimia 90 na zaidi[1]. Baada ya kusafishwa inafaa kusafirishwa katika mabomba kwa kilomita mamia au maelfu hadi pale inapogawiwa kwa watumiaji.

Kama hakuna mabomba pale gesi inapozalishwa gesi inabadilishwa kuwa gesi miminika, kwa kuipoza hadi sentigredi -161°C (chini ya sifuri). Katika hali hiyo gesi ni miminika inachukua nafasi ndogo tu. Husafirishwa kwa meli zinazobeba tangi zinazopoozwa na kupokewa katika bandari maalumu zenye vifaa vya kutunzia gesi hii baridi.

Remove ads

Chanzo cha gesi na petroliamu

(linganisha: Chanzo cha mafuta ya petroli)

Mara nyingi gesi asilia hutokea mahali pamoja na mafuta ya petroli (petroliamu) kwa sababu dutu hizo mbili zilitokea pamoja kwenye tako la bahari kutokana na viumbe vya algae na planktoni.

Bahari imejaa viumbe vidogo hivi ambavyo vinashuka chini hadi tako la bahari baada ya kufa. Huko haviweza kuoza kama kawaida kutokana na ukosefu wa oksijeni, hivyo hubadilika kuwa ganda la tope ogania. Baada ya miaka milioni ganda la tope hufunikwa na mashapo kama mchanga utakaokuwa mwamba. Chini ya funiko hilo tope ogania hupokea shinikizo kubwa pia joto na hivyo molekuli zinazojenga mwili wa algae hupasuliwa kuwa safu za hidrokaboni. Zile zilizo nzito zinakaa chini kama mafuta na sehemu nyepesi zinapanda juu ya mafuta kama gesi. Hapo gesi inashikwa na tabaka la mwamba imara linalozuia kupanda kwake. Kama tabaka la namna hiyo halipo hakuna gesi tena maana yote imeshapotea kwa kupanda juu na kuingia hewani muda mrefu uliopita.

Kikemia mafuta yale sawa na gesi asilia ni hasa mchanganyiko wa hidrokaboni mbalimbali lakini gesi huwa na molekuli nyepesinyepesi tofauti na mafuta yenye molekuli nzitonzito.

Chini ya ardhi gesi ambayo ni nyepesi hupatikana juu ya mafuta. Wakati akiba ya gesi na petroliamu chini ya ardhi hutobolewa kwa keekee gesi inatangulia kuondoka. Zamani makampuni yaliyotafuta petroliamu yalichoma gesi bila kuitumia lakini siku hizi thamani kubwa ya gesi imetambuliwa.

Gesi asilia inasafirishwa kutoka mahali inapopatikana ama kwa meli za pekee au kwa mabomba makubwa ya kimataifa.

Remove ads

Uzalishaji

Mnamo mwaka 2004 takriban mita za mjao bilioni 589 zilizalishwa. Zilitosheleza asilimia 24 za mahitaji ya nishati duniani. Nchi zinazozalisha gesi nyingi duniani kwa sasa ni Urusi na Marekani. Urusi ina pia akiba kubwa duniani maana kuna bado kiasi kikubwa sana ya gesi chini ya ardhi. Lakini nyingine zenye akiba kubwa ni nchi zilizopo kando ya Ghuba la Uajemi ambazo ni Uajemi, Qatar, Saudia na Falme za Kiarabu.

Gesi hukatamwa kwenye chanzo chake, kusafishwa halafu kusafirishwa kwa njia ya bomba hadi watumiaji au hadi bandari inapowekwa kwenye meli za tangi. Kwa kawaida gesi asilia ama hugandamizwa kuwa miminika kwa ajili ya usafirishaji kwenye mabomba.

Maelezo zaidi Nchi, Akiba zilizothebitishwa (millioni m³) ...
Remove ads

Matumizi

Gesi huchomwa kama chanzo cha nishati kwa matumzi ya kibinadamu. Inachoma kwa kuonyesha ulimi wa buluu ambao ni safi hauachishi gesi nyingi za machafuko hewani.

Matumizi yake ni hasa

  • Uzalishaji umeme: gesi inapasha maji moto kwa kuendesha rafadha ya kuzalisha umeme
  • Upishi: gesi asilia hupatika ama kwa bomba hadi kila nyumba au katika chupa za gesi
  • Ukanzaji wa nyumba katika mazingira baridi
  • Fueli ya magari
  • Aina za plastiki hutengewezwa kwa gesi asilia

Gesi asilia husafiwa kwa sababu inachangia kidogo tu kwenye machafuko ya mazingira hasa kupanda kwa halijoto duniani. Hata hivyo si fueli bila machafuko. Pia sawa na fueli kisukuu nyingine akiba zake zinazidi kupungua haraka.

Remove ads

Kurasa nyingine

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads