Qatar

From Wikipedia, the free encyclopedia

Qatar
Remove ads

Qatar, rasmi kama Dola la Qatar (kwa Kiarabu دولة قطر) ni nchi ndogo iliyoko katika Mashariki ya Kati kwenye pwani ya kaskazini-mashariki ya Rasi ya Uarabuni ikiwa na idadi ya watu takriban milioni 3, wengi wao wakiwa wahamiaji. Qatar inapakana na Saudia upande wa kusini na inazungukwa na Ghuba ya Uajemi upande mwingine. Ina jumla ya eneo la takriban kilomita za mraba 11,571, na hivyo kuwa moja ya nchi ndogo zaidi duniani.Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Doha, ambalo ni kituo kikuu cha kitamaduni na cha kiuchumi cha nchi hiyo.

Ukweli wa haraka Dola la Qatar دولة قطر Dawlat Qatar, Mji mkuu na mkubwa ...
Remove ads

Historia

Makala kuu: Historia ya Qatar

Maeneo ya Qatar, pamoja na Falme za Kiarabu na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao.

Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.

Remove ads

Siasa

Miaka ya mwisho Qatar imejihusisha na siasa ya Mashariki ya Kati kwa kuwapa silaha Waislamu wenye itikadi kali kama vile huko Palestina, Syria na Iraki, na hata Daish.

Kwa sababu hiyo imetengwa na nchi jirani, hasa Saudia.

Watu

Wananchi wengi wa Qatar kwa asili ni Waarabu na Waafrika (utumwa nchini ulichelewa sana kufutwa). Lakini kati ya wakazi wote, wenyeji hao ni asilimia 12 tu (313,000), yaani idadi kubwa sana si Waqatari wenyewe bali ni wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali, hasa Uhindi (zaidi ya 21%) na nchi za kandokando yake (Nepal 16.6%, Bangladesh 12.5%, Pakistani 4.5%, Sri Lanka 4.3%), halafu Ufilipino (10%), Misri (9%) n.k.

Kiarabu ni lugha rasmi ya nchi lakini Kiingereza hutumiwa mara nyingi kwa mawasiliano ya biashara na ofisini.

Waqatari wenyewe ni Waislamu (hasa Wasuni) lakini watu kutoka nje hufuata pia dini mbalimbali: hivyo kati ya wakazi wote 65.5% ni Waislamu, 15.1% ni Wahindu, 14.2% ni Wakristo, 3.3% ni Wabuddha n.k.

Uchumi

Uchumi wote wa Qatar una msingi wa mafuta ya petroli na gesi yake. Kwa wastani wakazi wake wana kipato kikubwa kuliko watu wa nchi zote duniani.

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Qatar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads