Bahari ya Kiarabu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bahari ya Kiarabu
Remove ads

Bahari ya Kiarabu (kwa Kiarabu: بحر العرب bahr al-arab) ni sehemu ya kaskazini ya Bahari Hindi iliyopo baina ya Bara Arabu na Bara Hindi. Eneo lake ni takribani kilomita za mraba 4,82,000 ilhali kina kirefu ni mita 4,652.[1].

Thumb
Bahari ya Kiarabu
Thumb
ramani ya Bahari ya Kiarabu

Upande wa kaskazini inapakana na Pakistan na Iran, upande wa magharibi na Omani, Yemen na Somalia, upande wa mashariki na Uhindi. Ghuba ya Aden iko upande wa magharibi-kusini na hapa mlangobahari wa Bab el Mandeb ni njia ya kuingia Bahari ya Shamu. Ghuba ya Oman inaunganisha na Ghuba ya Uajemi.

Mpaka wa kusini ni mstari baina ya rasi ya Bara Hindi hadi Rasi Guardafui kwenye Pembe la Afrika.

Mto mkubwa unaoishia humu ni mto Indus.

Visiwa si vingi, ni pamoja na Sokotra (Yemen), Masirah (Omani), Lakshadweep (Uhindi) na Astola (Pakistan).

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads