Gilbati wa Neuffonts
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gilbati of Neuffonts, O. Praem. (Auvergne, leo nchini Ufaransa, mwishoni mwa karne ya 11 - Saint-Didier-la-Forêt, Ufaransa, 6 Juni 1152) alikuwa mkabaila aliyeishi kama mkaapweke kwa miaka michache kabla hajajiunga na shirika la Wakanoni wa Premontree, na kufanywa abati.

Kabla ya kutawa alikuwa na mke na binti mmoja akashiriki katika vita vya Msalaba (1146). Baada ya kukubaliana na mwenzake wa ndoa, alianzisha monasteri ya kike huko Aubeterre iliyoongozwa kwanza na mke wake, halafu na binti yao. Alianzisha pia hospitali kwa ajili ya wakoma na monasteri ya kiume huko Neufforts[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Papa Benedikto XIII alithibitisha heshima hiyo tarehe 22 Januari 1728.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads