Goeriki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Goeriki (pia: Goheric, Goderic, Goëry, Goeric, Goericus, Goéry, Abbo, Appo, Abdo, Albo; Albi, leo nchini Ufaransa[1], 565/575 [2] - 643 hivi) alikuwa mwanajeshi mwenye cheo kikubwa[3] chini ya Dagobati I, mfalme wa Austrasia.

Baba wa mabinti wawili, ambaye mmojawao (Prisia) anaheshimiwa kama mtakatifu bikira, mwaka 627 alichaguliwa kuwa askofu wa Metz[4] baada ya Arnulfo, ambaye labda alikuwa jamaa yake na alimpa upadirisho, kwenda kwa siri kuishi kama mkaapweke karibu na monasteri ya Hamend iliyoanzishwa na rafiki yake Amato[5].
Arnulfo alipofariki, Goeriki alihamisha kwa heshima zote masalia yake mjini Metz [6].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Septemba[7].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads