Furukombe

From Wikipedia, the free encyclopedia

Furukombe
Remove ads

Furukombe, fukombe, kwazi, yowe au tai mlasamaki ni ndege mbuai wa nusufamilia Haliaeetinae katika familia Accipitridae.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Ndege hao ni baina ya tai wakubwa kabisa. Uzito wao unatofautiana kutoka kg 2 (furukombe wa Sanford) mpaka 9 (furukombe wa Steller).

Manyoya yao yana rangi ya kahawia mpaka nyeusi lakini kichwa, mkia, kidari na tumbo ni nyeupe kufuatana na spishi. Furukombe wa Madagaska, wa Sanford na wa Ulaya wana kichwa hudhurungi.

Spishi zote zinatokea karibu na maji ama baridi ama ya bahari. Hula samaki hasa lakini ndege wengine, mizoga na mara kwa mara wanyama wadogo pia.

Hujenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au mwamba. Jike hutaga mayai 1-3.

Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads