Hedwiga wa Polandi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Hedwiga wa Polandi
Remove ads

Hedwiga (kwa Kijerumani Hedwig; kwa Kipolandi Jadwiga, linatamkwa jadˈviɡa; Budapest, Hungaria, 1373/1374 - Krakov, Polandi, 17 Julai 1399) alikuwa malkia wa Polandi na Lituanya.

Thumb
Malkia Hedwiga leo anaheshimiwa kama mtakatifu.
Thumb
Ngao yake.
Thumb
Vazi maalumu la ibada la Jadwiga.

Kuanzia mwaka 1384 hadi kifo chake alitawala nchi ya Polandi akiitwa 'mfalme' badala ya 'malkia', ili kusisitiza kwamba hakuwa tu mke wa mtawala halisi[1].

Alizaliwa katika ukoo wa Wakapeti wa Anjou, binti wa mwisho wa mfalme Luis I wa Hungaria na Elizabeti wa Bosnia.[2].

Kwa kuolewa na Ladislaus wa Lituania, alimfanya abatizwe akaeneza Ukristo katika nchi hiyo ya Kipagani [3].

Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu na msimamizi wa kila malkia. Papa Yohane Paulo II ndiye aliyemtangaza rasmi mwenye heri tarehe 8 Agosti 1986 na mtakatifu tarehe 8 Juni 1997.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia[4].

Remove ads

Picha

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads