Horus

From Wikipedia, the free encyclopedia

Horus
Remove ads

Horus alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Katika mitholojia ya Kimisri alikuwa mwana wa Isis na Osiris. Aliabudiwa hasa kama mungu wa anga na pia mungu wa ufalme.

Thumb
Sanamu ya Horus kwa umbo la kozi huko Misri

Ibada yake iliendelea kwa muda mrefu, kuanzia nasaba ya kwanza hadi wakati wa Misri ya Kiroma. Katika kipindi hicho mawazo mengi kuhusu Horus yalitokea akaabudiwa kwa maumbo mengi tofauti.

Lakini umbo kuu lilikuwa ndege ya kozi au mwanadamu mwenye kichwa cha kozi.

Horus, aliabudiwa kote Misri, haswa huko Pe, Bendet na Khem .

Remove ads

Mwonekano

Horus alichukuliwa kuwa mzuri na kawaida alionekana kama kozi au mtu mwenye kichwa cha kozi, ingawa wakati mwingine alionekana kama mamba mwenye kichwa cha kozi. Kwa kawaida alivaa taji maradufu kuashiria utawala wake juu ya Misri yote na uhusiano wake kama mlinzi wa Farao.

Kazi

Horus alikuwa mungu wa anga na pia mungu wa vita. Kila farao wa Misri alitazamwa na kuheshimiwa kama Horus aliye hai. Alipofariki, farao aliendelea kutazamwa kama Osiris, mungu wa wafu na baba wa Horus. Farao mpya alikuwa Horus. Aliaminiwa anamlinda farao. Alikuwa mungu mlinzi, ambaye alikuwa mungu aliyepigana na uovu. Aliwakilisha haki.

Thumb
Sanamu ya Horus kwa umbo la binadamu mwenye kichwa cha kozi
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads