Human Nature
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
"Human Nature" ni wimbo wa R&B uliombwa na msanii wa rekodi za muziki wa Kimarekani, Michael Jackson. Wimbo huu ulitungwa na Steve Porcaro na John Bettis, na ulitayarishwa na Quincy Jones kwa ajili ya albamu yake ya sita ya Thriller (1982). Awali, Porcaro alirekodi demo kaseti ya majaribio ya wimbo huu, ambayo hiyo ndiyo baadaye alikuja kupewa Jones.
"Human Nature" ulitolewa mnamo tar. 3 Julai 1983, ukiwa kama wimbo wa tano katika albamu. Japokuwa wimbo haujatolewa nchini UK, wimbo ulipata mafanikio makubwa katika chati za US. Kwa kushika namba mbili kwenye chati za Billboard' Hot Adult Contemporary na namba saba kwenye chati za Hot 100. Wimbo huu ni wa tano wa Michael Jackson kutoka katika albamu ya "Thriller" na kuingia kwenye Kumi Bora'. Nchini New Zealand, single ilishika nafasi ya 11. Wimbo huu wa "Human Nature" ulikuja kuimbwa na kusampuliwa na wasanii kibao. Wasanii hao ni pamoja na: Miles Davis, SWV, Nas, Jason Nevins na Boyz II Men.
Remove ads
Chati zake
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads