Hunfridi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Hunfridi, OSB (alifariki Therouanne, Ufaransa wa leo, 871) alikuwa mmonaki aliyechaguliwa mwaka 856 kuwa askofu wa mji huo ingawa hakupenda.

Hali ilikuwa ngumu sana upande wa siasa, kutokana na uvamizi wa Wanormani walioteketeza mji, na upande wa Kanisa vilevile, kutokana na maadili kumomonyoka kabisa hata utawani.

Papa Nikola I alimhimiza aendelee na kazi yake, naye akakubali akawa faraja ya wananchi hadi kifo chake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Machi[1].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads