Papa Nikolasi I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Nikolasi I
Remove ads

Papa Nikolasi I au Nikolasi Mkuu (takriban 82013 Novemba 867) alikuwa Papa kuanzia tarehe 24 Aprili 858 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].

Thumb
Mt. Nikolasi I.

Alimfuata Papa Benedikto III akafuatwa na Papa Adriano II.

Anakumbukwa kwa kuimarisha kwa nguvu za kitume mamlaka ya Papa wa Roma katika Kanisa lote, akichangia ustawi wa cheo hicho, hasa katika Ulaya Magharibi[3]. Alisisitiza kuwa mamlaka hiyo iko juu ya watawala pia katika masuala ya imani na maadili.

Alikataa kutangaza ubatili wa ndoa ya mfalme Lothari II wa Lotharingia na mke wake, ingawa mfalme aliudai ili kumuoa Waldrada, mtaguso fulani uliukubali na jeshi la Wafaranki lilizingira Roma.

Mahusiano na Dola la Roma Mashariki yaliharibika kwa sababu aliunga mkono Patriarki Ignasi wa Konstantinopoli aliyekuwa ameondolewa madarakani ili kumpisha Fosyo.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 13 Novemba[4].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi

Tanbihi

Marejeo=

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads