Ignas Kim Chejun
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ignas Kim Chejun (aliteswa kikatili na kukatwa kichwa Seoul, 26 Septemba 1839) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe ni siku ya kifodini chake[2].
Waliouawa pamoja naye ni: Sebastiani Nam Igwan, Magdalena Ho Kyeim, Julita Kim, Agata Chon Kyonghyob, Charles Cho Shinchol, Magdalena Pak Pongson, Perpetua Hong Kimju, Kolumba Kim Hyoim[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads