Sebastiani Nam Igwan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Sebastiani Nam Igwan (aliteswa kikatili na kukatwa kichwa Seoul, 26 Septemba 1839) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[2].

Waliouawa pamoja naye ni: Magdalena Ho Kyeim, Julita Kim, Agata Chon Kyonghyob, Charles Cho Shinchol, Ignas Kim Chejun, Magdalena Pak Pongson, Perpetua Hong Kimju, Kolumba Kim Hyoim[3].

Remove ads

Mazingira

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads