Irene Tarimo
Mwanasayansi From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Irene Aurelia Tarimo (alizaliwa mwaka 1964) ni mhadhiri nchini Tanzania, na Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayansi ya Mazingira katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania [1]. Pia ni mwanasayansi na mtafiti katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania [2]. Alikuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Mkoa wa Lindi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa takribani miaka kumi.[3]
Remove ads
Wasifu
Irene alimaliza elimu yake ya awali ya msingi Rombo. Katika elimu yake ya sekondari alikuwa mwanafunzi katika shule ya wasichana ya Weruweru iliyopo mjini Kilimanjaro na baadae kujiunga kidato cha tano na sita na shule ya wasichana ya Kilakala iliyopo Morogoro. Alijiunga na Chuo cha Uwalimu cha Dar es Salaam (DUCE) na kusoma masomo ya Kemia, Biolojia na Taaluma. Alipomaliza alipata ajira ya uwalimu katika shule za sekorandari, Shule ya Sekondari ya Kifungilo, Shule ya Sekondari ya Morogoro, Shule ya Sekondari ya Weruweru na Shule ya Sekondari ya Mwika.
Mwaka 1995 alijiunga Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na mwaka 2003 alitunukiwa Shahada ya awali ya Sayansi katika Taaluma (B.Sc.Ed) kwa daraja la kwanza. Irene aliweka historia kwa kuwa mwanafunzi wa kwanza tangu miaka kumi ya kuanzishwa Chuo Kikuu Huria mwaka 1992 kupata Alama ya daraja la kwanza. Alipata zawadi kutuka kwa Makamo Mkuu wa chuo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Irene alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya Shahada ya pili ya Uzamili katika Sayansi ya Mazingira na kuhitimu mwaka 2007. Baadaye alijiunga tena na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa Shahada ya tatu ya Uzamivu akishirikiana na Chuo Kikuu cha Copenhagen mpaka kumaliza kwake mwaka 2013.
Remove ads
Kazi
Daktari Irene amekuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Mkoa wa Lindi kwa takribani miaka tisa tangu 2007 amewezesha shughuli za chuo ukanda wa Mikoa ya kusini mwa Tanzania kufanikiwa kwa ustadi na uadilifu mkubwa.[4] Amewezesha kituo cha Lindi kupata eneo la Ardhi takribani Ekari 100 kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa makazi mapya ya kituo cha chuo. Pia alifanikisha upatikanaji wa Ekari takribani 3 kwa ajili ya maonyesho ya Nane Nane eneo la Ngongo, Mkoani Lindi [5]. Alifanikisha harambee ya upatikanaji gari la usafiri wa chuo na kwa shughuli nyingine mbalimbali za chuo [6].

Remove ads
Machapisho
Irene Aurelia Tarimo ameandika machapisho kadhaa juu ya Sayansi na mambo ya kijamii:
- Kuondolewa kwa Takataka na utumiaji wa tena wa Maji yaliyopangwa kutoka Mabwawa ya Udhibiti wa taka ya Mattera (MWSPs)
- Model ya Kiikolojia na Uhandisi wa Maziwa na Viunga
- Mfano wa Matibabu ya Maji taka ya Manispaa katika Mfumo unaojumuisha Mabwawa ya Udhibiti wa Taka, Mifereji Iliyojengwa na Mabwawa ya Samaki nchini Tanzania
- Sura ya 23 - Mfano wa Matibabu ya Maji taka ya Manispaa katika Mfumo unaojumuisha Mabwawa ya Udhibiti wa Taka, Mifereji Iliyojengwa na Mabwawa ya Samaki nchini Tanzania
- Model ya Kiikolojia na Uhandisi wa Maziwa na Viunga
- Ubora wa Maji Yanayorudishwa na Kuhifadhiwa upya Carp Carp katika Mabwawa ya Akiba ya Kupokea Maji ya Manispaa Iliyopatikana: Matokeo kwa Afya ya Binadamu Ilihifadhiwa 3 Julai 2020 kwenye Wayback Machine.
- KUUFUNDISHA NA KUJIFUNZA KWA OVI ZA UWEZO WA MFIDUO WA ODL Ilihifadhiwa 17 Aprili 2023 kwenye Wayback Machine.
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads