Isdory Tarimo
Mkulima, Mwanasiasa na Mwanamazingira From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Isdory Lucas Tarimo (amezaliwa 15 Novemba 1954) ni Mtanzania mwanamazingira, mwanasiasa na mkulima kutoka Mkoa wa Kilimanjaro.
Remove ads
Maisha ya awali na kazi
Tarimo ni mwanasiasa mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Mapinduzi CCM. Kabla ya Serikali kugawanya kata ya Nanjara-Reha iliyokuwa na wakazi takribani 26,000, alichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Nanjara-Reha, Wilaya ya Rombo kwa mwaka 2000 hadi 2010.[1] [2] [3] [4] [5] Pia ni mwanaharakati wa mazingira akisimamia Taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughulika na mazingira, Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Tanzania (Tecoso Tanzania).[6] [7] [8]
Remove ads
Shughuli za Kilimo na Utumishi wa Umma
Tarimo ni Katibu Mkuu wa Shirika la Taifa la Wakulima Tanzania, Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) akiwakilisha tawi la Mkoa wa Kilimanjaro (MVIWAKI).[9] Mwaka 2022, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Society - TASO) akiwakilisha mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Mkoa wa Manyara, Mkoa wa Arusha na Mkoa wa Kilimanjaro.[10]
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads