Isidori wa Pelusio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Isidori wa Pelusio (kwa Kigiriki: Ἰσίδωρος ὁ Πηλουσιώτης; alifariki 450 hivi) alikuwa mmonaki padri wa Misri.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Februari[1].
Maisha
Mtoto pekee wa familia maarufu wa Aleksandria[2], akiwa ameshajipatia ujuzi mwingi, alitawa kwenye mlima karibu na mji wa Pelusium, kwa kufuata nyayo za Yohane Mbatizaji na Mababu wa jangwani [3].
Pia alijitosa kuhubiri kwa mfano wa Yohane Krisostomo akamtetea dhidi ya dhuluma kutoka kwa patriarki Theofilo wa Aleksandria, ndugu yake, na kwa malkia Eudosia.
Maandishi
Anajulikana kwa barua 2,000 hivi alizowaandikia patriarki Sirili wa Aleksandria, kaisari Theodosius II na wengineo wengi.[4] Baadhi yake ni muhimu kwa ufafanuzi wa Biblia.[5]
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads