Jehanum
From Wikipedia, the free encyclopedia

Jehanum ni neno lenye asili ya Kiebrania (גיא בן הינום, Gei Ben-Hinnom, "bonde la mwana wa Hinnom"; kwa Kigiriki: γέεννα) linalomaanisha adhabu ya moto wa milele ambayo kadiri ya Biblia na Kurani itawapata watu waovu huko ahera kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu.
Kwanza Gehinnom (גהנום/גהנם) ni jina la bonde karibu na Yerusalemu lililotazamwa kama laaniwa (Yer 7:31, 19:2-6) kwa sababu ya maovu yaliyotendwa huko, hasa kuchinja watoto kwa heshima ya miungu.
Hata hivyo katika Agano Jipya jina hilo linatumika zaidi kwa maana ya moto wa milele[1], pia kwa sababu wakati wa Yesu bonde hilo lilitumika kama jalala, hivyo moto uliokuwa wa kudumu ndani yake. Katika Injili imeandikwa mara 11 kwamba mwenyewe alitumia jina hilo [2] kudokezea hali iliyo kinyume cha uzima wa milele[3].
Yesu alizungumzia moto wa milele, huku akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee. Alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo: “Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake” (Math 25:41). “Humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki” (Mk 9:48). “Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku” (Ufu 14:11).
Katika Uislamu pia moto wa milele unaitwa جهنم, Jahannam[4]. Kurani inaitaja mara 77 kumbe haitaji kamwe kuzimu (هيدز).
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.