Jeradi Edwards
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jeradi Edwards (pia alijiita: Edward Campion; Ludlow, Shropshire, 1552 – Canterbury, 1 Oktoba 1588) alikuwa padri kutoka Uingereza.

Baada ya kupewa upadrisho huko Ufaransa (1587), alirudi nchini ili kufanya utume kwa siri ila alikamatwa na, baada ya kufungwa gerezani muda mrefu, hatimaye alinyongwa pamoja na mapadri wenzake Robati Wilcox na Kristofa Buxton na mlei Robati Widmerpool aliyesaidia utume kama huo wakati wa dhuluma ya malkia Elisabeti I[1].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu na Papa Paulo VI mwaka 1976.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Oktoba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads