Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam (kwa Kilatini Archidioecesis Daressalaamensis) ni mojawapo kati ya majimbo 36 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Zanzibar, Tanga, Morogoro, Mahenge, Ifakara, na Bagamoyo.
Askofu mkuu wake ni Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, O.F.M.Cap.
Remove ads
Historia
- 16 Novemba 1887: Kuanzishwa kwa Prefekturi ya Kitume ya Dar-es-Salaam kutokana na Vikarieti ya Kitume ya Nairobi
- 15 Septemba 1902: Kupandishwa hadhi kuwa Vikarieti ya Kitume ya Dar-es-Salaam
- 25 Machi 1953: Kufanywa dayosisi (jimbo kuu)
- 7 Machi 2025: Kumegwa ili kuzaa Jimbo la Bagamoyo
Uongozi
- Maaskofu Wakuu wa Dar-es-Salaam
- Yuda Thaddeus Ruwa'ichi (tangu 2019)
- Kardinali Polycarp Pengo (1992 - 2019)
- Kardinali Laurean Rugambwa (1968 – 1992)
- Edgar Aristide Maranta OFMCap (1953 – 1968)
- Vikari ya Kitume wa Dar-es-Salaam
- Edgar Aristide Maranta OFMCap (1930 – 1953)
- Joseph Gabriel Zelger OFMCap (1923 – 1929)
- Thomas Spreiter OSB (1906 – 1920)
- Cassian Spiß OSB (1902 – 1905)
- Prefekti ya Kitume wa Dar-es-Salaam
- Padri Maurus Hartmann OSB (1894 – 1902)
- Padri Bonifatius Fleschutz OSB (1887 – 1891)
Remove ads
Takwimu
Baada ya kumegwa, eneo la jimbo lina kilometa mraba 39,849, ambapo kati ya wakazi 6,907,307 Wakatoliki ni 1,800,395 (sawa na 26.1%).
Parokia ziko 147, zikihudumiwa na mapadri 365 (110 wanajimbo na 255 watawa), watawa wanaume wasio mapadri ni 42. Masista kabla ya jimbo kumegwa walikuwa 669.
Viungo vya nje
- Catholic Hierarchy (Kiingereza)
- www.gcatholic.org (Kiingereza)
![]() |
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads