Joji Preca
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Joji Preca (kwa Kimalta: Ġorġ; La Valletta, Malta, 12 Februari 1880[1] - Santos Vendroob, Malta, 26 Julai 1962) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Malta aliyeshughulikia hasa malezi na katekesi ya vijana[2]. Kwa ajili hiyo alianzisha Shirika la Mafundisho ya Kikristo ili kuonyesha Neno la Mungu linavyofanya kazi ndani ya taifa lake.

Ndiye aliyebuni mafumbo ya mwanga ya Rozari[3].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza kuwa mwenye heri tarehe 9 Mei 2001[4], na Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 3 Juni 2007, wa kwanza kutoka nchi hiyo ya Ulaya visiwani[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads