Joyce Lazaro Ndalichako
Mwanasiasa wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Joyce Lazaro Ndalichako (alizaliwa Musoma, 21 Mei 1964) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha CCM. Aliteuliwa[1] na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwa mbunge na pia Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa miaka 2015 – 2020 nchini Tanzania[2] akiendelea hata katika awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan.

Remove ads
Elimu yake
Joyce Ndalichako alipata shahada yake ya kwanza katika Ualimu (kwa Kiingereza: Bachelor of Science with Education, majoring in Mathematics), akijikita katika Hisabati, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania mnamo mwaka 1987 hadi 1991. Alipata shahada yake ya Uzamivu katika Saikolojia ya Elimu (Kiingereza: PhD in Educational Pyschology, major in Educational Statistics & Measurement and Evaluation), akijikita katika Takwimu za Kielimu na Vipimo vya Kielimu pamoja na Tathmini ya Elimu, katika Chuo Kikuu cha Alberta nchini Kanada. [3]
Remove ads
Kazi yake
- Mnamo mwaka 2000 hadi 2005, Joyce Ndalichako alikuwa ni mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akifundisha masuala ya Vipimo vya Kielimu na Tathmini ya Elimu, mbinu za Utafiti na Takwimu za Kielimu, huku akisimamia kazi (Kiingereza: dissertation) za wanafunzi wake.[4][3]
- Kuanzia mwaka 2014 hadi leo, Joyce Ndalichako ni profesa msaidizi na mkuu msaidizi kwa upande wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Taasisi ya Maendeleo ya Elimu, Afrika Mashariki.[3][4]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads