Juba ya chini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Juba ya chini (Kisomali: Jubbada Hoose, Kiarabu: جوبا السفلى, Kiitalia: Basso Giuba) ni mkoa wa kiutawala (gobol) kusini mwa Somalia.[1]

Makao makuu yake yakiwa Kismayo, kwenye autonomous Jubaland.

Una misitu ya kijani na wanyama pori kama simba, twiga, viboko, mamba na fisi.

Juba ya kusini imepakana na Kenya, Mkoa wa Kisomali wa Gedo, Juba ya kati (Jubbada Dhexe), na Bahari ya Somalia. Mkoa huu umepewa jina kufuatia  Mto Jubba unaopita katikati yake na kuishilia kwenye Bahari ya Somalia katika Goobweyn.  

Hifadhi ya taifa ya Lag Badana ipo katika Juba ya kusini

Remove ads

Historia

Kuanzia mwanzo wa historia mpaka karne ya 19, Juba ya chini imekua ikikaliwa na ukoo wa Hawiye claw ambao ndio wakaaji wakubwa kusini mwa. Ijapokua ,baadae katikati ya karne ya 20, fa,ilia chache za Darod zilianza kuishi katika mji wa Kismayo. Kufikia mwisho was karne ya 20, kama wageni, walikwisha anzisha sehemu ndogo za kibiashara. Mwanzoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia, Kismaio ikifahamika kama  Waamo ilikumbwa na uharibifu mkubwa miongoni mwa viongozi wa vikundi sana sana kati ya Hawiye na Darod kila mmoja akidai umiliki wa mikoa ya Juba ya chini na kati. Ila kwa upande mwingine, Mji ulikua kiuchumi kufikia kuwa eneo kubwa la biashara ya mifugo.[2] Wawakilishi wakuu kujianzisha kismayo walikua  Majeerteen wafanya biashara kutoka Kaskazini Ras Hafun wenye hadhi, waliotabulika kama Hafuuni. Katika miungo miwili ya kwanza ya karne ya 20, wakati wa upinzani wa Mohammed Abdullah Hassan ("Mad Mullah") Dervish wafuasi wa ukoo mdogo wa Dhulbahante walijiunga pia[3]

Miongoni mwa vitu vingi, mikoa yote inaonekena kukaliwa na familia zisizo za wakazi asili kuanzia mwanzo wa muundo shirikishi ndani ya nchi nzima.   Kati ya  1974 na 1975,ukame mkubwa uliojulikana kama Abaartii Dabadheer ("Ukame Lingering ") ulitokea  kaskazini mwa Nchi ya Somalia. Umoja wa Kisoviet, amboa kwa wakati huo ulikua na mahusiano ya kimkakati na  serikali ya the Siad Barre, uliwachukua watu wake wapatao  90,000 kutoka katika maeneo yaliyoharibiwa na ukame ya Hobyo na  Caynaba. Makazi mapya madogo yaliyojulikana kama Danwadaagaha ("makazi jumuishi") yalianzishwa katika mikoa ya Jubbada Hoose (Jubba ya chini) na Jubbada Dhexe (Jubba ya kati). Familia zilizosafirishwa walijuzwa juu ya njia za kilimo na uvuvi, mabadiliko kutoka kwenye njia zao za jadi za ufugaji na uchungaji wa mifugo.

Remove ads

Wilaya

Juba ya chini inaundwa na wilaya tano:[4]

  • Wilaya ya Afmadow
  • Wilaya ya Badhaadhe
  • Wilaya ya Kismaayo
  • Wilaya ya Jamaame
  • Wilaya ya Xagar

Visiwa vya Bajuni vipo ndani ya mkoa huu pia.

Miji mikubwa

Maelezo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads